2015 Tutegemee Makubwa, Diamond aanza kukubalika Kimataifa

 


Ni mwaka mmoja sasa umepita tangu Diamond aime na Msanii Davido kwenye remix ya wimbo wa Number One. Ikumbukwe kuwa mwaka mmoja huo ilikua ni Diamond ndio anatafuta nafasi ya kufanya kolabo na Wasanii wakubwa wa Nigeria ambao wamekua kwenye headlines za kuitawala Afrika kupitia muziki wao.

Sasa baada ya kolabo na Davido kwenye ile ‘number one rmx’ milango ikaanza kufunguka, alipofanya kolabo na Iyanya ndio kabisa nguvu yake ikaongezeka ila kushinda tuzo 3 za Channel O Jumamosi ya November 29 2014 ndio Diamond akaingizwa rasmi kwenye list ya mastaa wa muziki Afrika kwa kuvunja rekodi ya Afrika Mashariki na kuwa wa kwanza kuwahi kushinda tuzo tatu kwa mkupuo on Channel O.

Wasanii wakubwa kutoka nchi za Nigeria, Congo, Uganda wameonesha nia ya kutaka kufanya Collaboration naye hasa baada ya kuona unyama alio ufanya kwenye wimbo wa Number One Remix. Hakika tutegemee Colaborations Nyingi kwa mwaka 2015 kwani Diamond ni wamoto haswa. 

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi