Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John pombe Magufuli leo amekutana na wakulima na wafanya Biashara wa zao la korosho kutokana na sinto fahamu iliyo jitokeza kuhusu bei ya zao hilo muhimu katika uchumi wa Tanzania ambapo mheshimiwa rais alitoa msimamo wake akiiwakilisha serikali lengo likiwa ni kulipa zao hilo thamani inayo stahili huku mkulima akifaidika na jasho lake.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Wanunuzi wa zao la Korosho katika kikao kilichofanyika katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere jijini Dar es Salaam na kutoa msimamo wa Serikali kuhusu bei ya Korosho kuwa isipungue shilingi 3000 kwa kilo moja.
Wadau na Wanunuzi wa Korosho wakiwa wanasikiliza Maelekezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati alipokutana nao na kuzungumza nao jijini Dar es Salaam.