Ali choki asinifikirie, Aendelee na mambo yake -Asha Baraka

 Baada ya msanii wa mziki wa Dance Ali Choki kupiga stori na eNEWZ wiki chache zilizopita na kusema mwaka 2018 atafanya kazi zake mwenyewe kama Mama Asha Baraka ataendelea kulala, kiongozi huyo wa Twanga Pepeta amemjibu Choki.

Mama Asha Baraka baada ya kusikia kauli hiyo  amesema anamshangaa sana Ali Choki kusema maneno hayo kwani tangu mwaka jana alishamruhusu akafanye kitu anachotaka hata kama ikiwa ni pamoja na kazi zake binafsi.

''Namshangaa sana Ali Choki mimi nishampa ruhusa afanye kazi nyingine yoyote bila kujali mkataba wetu unasemaje hivyo yeye aendelee na mambo yake wala asinifikirie'' amesema.

Asha Baraka pia amesema kuwa hataki Ali Choki afie Twanga Pepeta hivyo kama ana uwezo arudi akaifufue  Extra Band kwani alimpa uongozi ndani ya Twanga Pepeta akashindwa kuiongoza.

Ali Choki tayari ameshaonekana akiingia  studio na msanii Beka Flavour kuandaa kazi zake binafsi hivyo huenda akawa tayari ameshajiandaa na maisha bila ya Twanga Pepeta. Zaidi tazama eNEWZ ya EATV.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi