Kutokana na mashindano yaliyo fanyika nchini GHANA yakihusisha watu, makampuni na Taasisi zilizo anzishwa na vijana mbali mbali katika kutatua changamoto zinazo likumba bala la Africa Taasisi ya elimu ya NLab Innovation Academy ilijinyakulia Tuzo katika kipengele cha mtoa elimu mwenye kuongeza thamani.
Tuzo hizo zilitolewa tarehe 9 mwezi wa 11 mwaka 2018, zilipokelewa na Gloria Clement ambaye ni Mshauri wa mambo ya Biashara, Uwekezaji na Mafunzo katika chuo hicho ambaye. Mara baada ya kupokea Tuzo hiyo, Gloria alipata nafasi ya Kuzungumza na kuweza kuweka bayana mipangoi ambayo chuo hicho kimejiwekea katika kutatua changamoto za ajira huku kikiongeza thamani katika mafunzo wanayo yatoa ili yaweze kumsaidia mwanafunzi husika baada ya kupokea mafunzo hayo.