Usalama wa nchi wamfanya Raisi Uhuru Kenyatta kubadilisha balaza la mawaziri

 


Baada ya nchi hiyo kuelemewa na mashambulizi mara kwa mara na shinikizo la wananchi Rais Uhuru Kenyatta amemwachisha kazi  Waziri wa Usalama Joseph Ole Lenku na kumteua Waziri mpya wa Usalama Joseph Nkaiseri, kuchukua nafasi hiyo huku  Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyoakilazimishwa kuachia ngazi.

Baada ya lile shambulio la siku kumi zilizopita ambapo kundi la Al Shabaab liliwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri kwa basi kutoka Mjini Mandera karibu na mpaka wa Somalia, Kimaiyo na Ole Lenku wamekuwa wakikabiliwa na shinikizo za kujiuzulu kufuatia kukithiri kwa mashambulizi ya kigaidi na kuhatarisha  usalama, ambapo jana Novemba 02 wachimba kokoto 36 wameuawa na kikundi cha Al Shaabab katika kaunti ya Mandera.

… Hapa ni mahali tukemekaa kama mimi mwenyewe nimekaa miaka tisa ile mambo nashuhudia saa hii sijawahi jionea na macho yangu watu kuuliwa sijawahi ona, by the way maisha yetu iko hatarini…

“...Nakimbilia usalama wangu juu nahofia pale kwa nyumba hujui watavamia lini  watakuja lini, saa ndio natoka kwangu kwa nyumba nakaa nakuja kukaa hapa kulingana na ile mazingira tunayo  nakaa hapa kupata ulinzi wa Serikali inakuwa ni ngumu sana, sisi ndio tunafanya msituni tulio eneo la hapa Mandera Town wavamivi wanavyokuja wanapita njia za misituni sasa Polisi kujua ni ngumu…

Rais Kenyatta amesema kuwa baada ya mazungumzo na Kimaiyo alikubali kustaafu mapema kwa sababu zake binafsi.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi