Rayvanny Kuiwakilisha Tanzania Vymea - MTV EMA 2021




Leo sio siku ya mapumziko lakini Taifa linasherehekea rekodi nyingine iliyowekwa na Kijana wa Kitanzania kutumbuiza juu ya moja ya majukwaa makubwa ya burudani duniani, ni yuleyule Mkali toka WCB, President wa NLM….. Chui a.k.a Rayvanny ambaye ametumbuiza kwenye Tuzo kubwa Ulaya za MTV EMMA 2021.

Vannyboy ame-perform “tetema’ na Staa wa Colombia aitwae Maluma kwenye usiku wa utoaji wa tuzo za MT EMA 2021 kwenye Mji wa Budapest Hungary ambazo baadhi ya walioshinda Tuzo hizo ni pamoja na Nicki Minaj na Wizkid.

Maluma ni Staa wa muziki kutoka Colombia ambaye muziki wake umekuwa mkubwa sio kwa Colombia peke yake bali sehemu mbalimbali duniani na kumfanya awe miongoni mwa Wasanii ambao nyimbo zao zinafika mbali kila wanapozitoa huku hadi sasa akiwa na Followers milioni 59.7 kwenye Instagram pekee.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi