HABARI zilizopatikana hivi punde zinasema kuwa Jeshi la Polisi limesitisha kufanyika kwa mazishi ya aliyekuwa Mnenguaji wa bendi za African Stars 'Twanga Pepeta' Aisha Madinda,ili kufanya uchunguzi wa kina juu ya kifo chake.
Akihojiwa katika kipindi cha XXL, mtoto mkubwa wa marehemu alisema wamekubaliana na serikali wafanye uchunguzi wa kinaili hata kama akizikwa basi azikwe ikifahamika kipi kilichomuua, kwa sababu mama yake hakuwa mgonjwa kabla ya kukumbwa na mauti.Tangu jana baada ya kusambaa kwa kifo cha mnenguaji huyo aliyepitia makundi mbalimbali kabla ya kutua katika shoo za bendi, kulikuwa na maelezo ya kutatanisha juu ya kifo chake na mtoto huyo wa marehemu, aitwaye Feisal Mbegu alinukuliwa kuwa mama yake hakuwa mgonjwa na aliwasiliana naye jana yake akiwa buheri wa afya.
Inaelezwa kuwa mwili wa Aisha Madinda ulipelekwa hospitali ya Mwananyamala akiwa keshafariki na mwanamke mmoja anayetajwa kuwa rafikie aitwaye, Samira, huku ikielezwa kuwa aliondoka kwao KIgamboni ili kwenda kwenye mazoezi ya bendi ya Twanga Pepeta ambapo hata hivyo uongozi wa bendi hiyo umekana msanii wao huyo wa zamani kuwahi kwenda kufanya mazoezi kwao.
Awali mazishi hayo yalipangwa kufanyika leo nyumbani kwa wazazi ao, Kigaamboni.