Hatimaye msanii SHILOLE avishwa pete ya uchumba kwenye Birthday yake

 


Hayawi hayawi sasa yanakaribia kuwa. Wanamziki wawili ambao wamekuwa wakichukua vishwa vya habari kwa mapenzi yao moto moto hatimaye wamevishana pete ya uchumba yenye kuashiria ndoa ipo njiani. Wasanii hao ni Nuhu Mziwanda na Shilole.

Kwenye list ya mastaa wa Bongo Fleva walio katika uhusiana ya kimapenzi basi lazima couple hii uhusishe ambayo Dec 20 imeingia katika hatua ya juu baada ya Nuh Mziwanda kumvisha pete ya uchumba Zuwena Mohamed aka Shilole.

Tukio hilo special  la wapenzi hao wawili lilifanyika usiku wa kushereherekea siku ya kuzaliwa kwa msanii wa Bongo Fleva Shilole ambaye aliwaalika ndugu,jamaa na marafiki mbalimbali wakiwemo wasanii wenzake.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi