Bado wapenzi wa burudani ya muziki wa dansi nchini Tanzania wamegubikwa na majonzi ya kumpeteza msanii Asha Madinda.
Mtoto wa Marehemu Aisha, anaitwa Feysal Madinda akiwa makaburini
Jana ndio siku ambayo yalifanyika mazishi ya aliyekuwa mnenguaji wa Bendi ya Twanga Pepeta, Aisha Madinda katika makaburi ya Kibada, Kigamboni Dar es Salaam baada ya uchunguzi wa postmortem kukamilika katika Hospitali ya Muhimbili.
Watu mbalimbali walijitokeza kumsindikiza msanii huyo kwenye safari yake ya mwisho duniani, unaweza kuona matukio yote kwenye picha hizi.
Mwili wa asha Ukitolewa kwenye gari
Mwili wa Aisha Madinda ukiwasili nyumbani kwa ajili ya kuswaliwa kabla ya mazishi yaliyofanyika jana jioni katika makaburi ya Kibada, Kigamboni jijini Dar es salaam