Mwandishi wa Habari wa kituo cha Telemundo, Andres Herrera alivamiwa na kupigwa na mtu mmoja mjini California, nchini Marekani wakati akiendelea na majukumu yake ya kutafuta habari mtaani.
Jamaa huyo alimuuliza Herrera kama anafanya kazi ya uandishi wa habari, alipomjibu ‘ndiyo’ jamaa alimsogelea na kuanza kumpiga kipigo cha mbwa mwizi huku wakirekodi video.
Polisi wamesema jamaa ambaye amefanya kosa hilo tayari ana mashtaka mengine ambayo anakabiliwa nayo yakimhusisha na matumizi ya pombe na dawa za kulevya. Hali hii haipo nchi za wenzetu pekee, hata barani Africa kunmekuwa na tabia ya namna hii ambayo inapandikiza uoga katika baadhi ya waandishi na kupelekea kuwa ni kero katika tasnia ya Habari.