Nuh Mziwanda Amuomba Radhi Mume Wa Shilole

 IKIWA ni siku chache tangu msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda kudai kuwa bado anampenda aliyekuwa mpenzi wake, Shilole ijapokuwa ana mme tayari na kuibua mijadala mitandaoni na kwenye vyombo vya habari, staa huyo ameibuka na kuomba radhi.

 


Hivi karibuni Msanii Nuh Mziwanda aliongea kwa uchungu akisema “Bado nampenda SHILOLE nimeshindwa ku-move on, moyo wangu uko kwake’ Ikimaanisha kwamba ingawa walisha vishana pete, mambo yakayumba na kisha wakatengana kwa tambo kadha wa kadha, bado Nuhu anamapenzi kwa x wake huyo.

 

Sasa kupitia Empire ya EFM, akijibu swali la mtangazaji B Dozen, kama anahisi kuachana kwake na Shilole kumempunguzia mashabiki, Mziwanda amesema hapana, kwani anaamini mashabiki zake wamempendea muziki anao ufanya na si kwasababu alikuwa kwenye mahusiano na Shilole.

 

Akijibu swali kuhusu anachokifanya kuhusu Shilole haoni kama kina hatarisha ndoa ya Shishi na kumkosea Rommy ambaye ni mume wa Shishi.

 

Nuh ametumia fursa hiyol kumuomba Radhi, Rommy kama atakuwa anakerekwa na alichokiongea kuhusu mkewe, lakini atambue anacho kiongea haongei kwa lengo baya la kutaka wao wagombane au ndoa yao ivunjike, bali anaongea kwa kuwa ni hisia zilizo baki moyoni mwake na kuogeza kuwa anaiheshimu na kupenda ndoa ya Shilole.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi