Mwanamke Wa Mfano kwa mwaka 2024 - Carolyne Ekyarisiima

Anaitwa Carolyne Ekyarisiima kutoka Tanzania ambaye tangu mwaka 2010 amekuwa mstari wa mbele katika kuhakikisha mabinti wanakuwa kwenye mikono salama haswa linapo kuja swala la elimu na maisha kwa ujumla.  Amefikaje hapo na kwa nini awe yeye? Ungana nami mwandishi wako katika kukujuza.

Mwaka 2013 Tanzania iliingia kwenye orodha ya washindi wa tuzo za WSIS zilizo fanyika nchini Uswisi ambapo Taasisi kutoka tanzania ijulikanayo kwa jina la Apps and Girls iliweza kujinyakulia tuzo hiyo miongoni mwa washiriki shindani walio kuwa wakiishinania tuzo huyo kubwa na muhimu.

Ushindi huu ulishuhudiwa na Naibu waziri wa habari na mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mheshimiwa Kundo A. Mathew.

Naibu waziri akimpongeza mshindi wa tuzo za WSIS kutoka taasisi ya Apps and Girls Tanzania Bi. Carolyne Ekyarisiima, katika kipengele cha ajira kwa njia ya mtandao kupitia mradi wao wa ujasiriamali kwa wasichana kupitia TEHAMA.

Tuzo hizo zimetolewa kwenye kongamano la Jumuiya ya Habari na Mawasiliano Ulimwenguni (WSIS),lililo fanyika jijini Geneva , Uswizi kuanzia tarehe 13 hadi 17 Machi, 2023 kwa lengo madhubuti la kujadiliana na kuweka mikakati ya kuendelea kuboresha sekta ya habari na Mawasiliano kupitia TEHAMA.

Alianzaje anzaje?

Carolyne anasema alianza kufanya anacho kifanya mwaka 2010 ingawa rasmi kabisa alianzisha taasisi hii mwaka 2013 mwishoni ambapo lengo kubwa likiwa ni kuwasaidia mabinti kuweza itambua njia iliyo njema kwenye mambo ya TEHAMA kwani ndiko dunia ilipo kuwa inaendelea.

"Haikuwa rahisi kufanya haya, kwani ilikula muda na pesa na ilikatisha sana tamaa ikizingatiwa kuwa shule nyingi tulizo kuwa tuna fanya nazo kazi hazikuwa na vitendea kazi. kumbe wakati mwingi wanafunzi mabinti kwa wavulana walikuwa wakinya nyumbani kwangu na kufanya nao mafunzo sebuleni.

Mwanzo ilikuwa ngumwa kwa watu wa karibu kuelewa malengo yetu, ila tulipiga moyo konde kwani tuliamini kwamba tufanyacho kina kwenda kuzaa matunda huko mbele ya safari."

Ni program gani iliyo pata hii tuzo?

Katika taasisi ya Apps and girls kuna program nyingi, Mfano kuna:-,

1. Adalace program:maalumu kwa wanafunzi walio maliza chuo na hawajapata ajira. wanafunza mwafunzo ya TEHAMA na akili bandia ili kuweza ongeza sifa na ujuzi wa kuweza ajirika.

2. Jovia Program: Maalumu kwa mabinti ambao hawakubahatika kumaliza elimu kwa sababu mbali mbali mbali. Program hii ilianza mwaka 2019 ambapo ilikuwa imeshikwa mkonio na DTBI na SAIS.

3. Robotics: haya ni mafunzo ya kutengeneza roboti

4. Girls Entreprenuership Summit: Mkutano na mafunzo ya wanafunzi yenye kuwasaidia kutengeneza miradi na kuiwasilisha kwa hadhira.


Tuzo hii ni maalumu kwa mradi wa Jovia ambao kwa sasa unadhaminiwa na Tigo Tanzania. Carolyne anasema Jovia ni jina la mama yake mzazi ambaye wakati wa ujana wake alikuwa na ndoto ya kuwa msomi mkubwa, ila kutokana na changamoto za kiuchumi hakuweza endelea na masomo na hivyo kuishia kulima na kuwa mfanya biashara wa mazao ya kilimo hasa Ndizi.

Zaidi ya Tuzo Hii, Carolyne binafsi anatuzo zaidi ya Saba ambazo zote zimekuja kwa lengo la kukubali kile anacho kifanya. Tuzo hizo ni pamoja na:-

ngeza yeye binafsi na Timu yake nzima.

  1. Tigo Digital Changemakers Award - 2017
  2. Malkia wa Nguvu (2017) By Clouds Media Group
  3. The next generation of Leaders (2017) By IFA FOUNDATION 
  4. Innovator of the Year Award By Aid & International Development Forum
  5. 35 Most Influential Women in Tech By CIO Africa (Alitajwa)
  6. Digital Female Leader Awards (2019), Social Hero By Der DFLA (Aliteuliwa)
  7. 50 Most influential Young Tanzanians (2019) By Avance Media (Alitajwa)

Kama haitoshi, Taasisi yake ya Apps and Girls nayo imekuwa ikinyakuwa tuzo kadha wa kadha katika medani za kimataifa kutokana na shughuri nzuri inayo fanya katika kuwanyenyua watanzania. Tuzo hizo ni pamoja na :- 

  1. Social Inclusion Award (2019) By Women in Tech
  2. WSIS Prize (2020) Champion in Capacity Building by ITU 
  3. 1st runners up for the ATU Africa Innovation challenge (2021) By African Telecommunication union and ITU
  4. Overall winner of the ICT awards (2021)  By the Tanzania ICT commission
  5. Best ICT Incubator of the year (2021) By the Tanzania ICT commission
  6. Global Winner in E-Employment (2023) By WSIS
  7. Entrepreneurship Education Program Award (2023) By ASEB UNSUNG HERO

Kutokana na haya yote, Carolyne ni mmoja wa Wanawake ambao wamesaidia kuinua kiwango cha mapenzi na matumizi salama ya Sayansi ya Computer, habari na mawasiliano kwa mabinti na wanawake. 

Kwa sasa anafanya Shughuri Gani?

Zaidi ya kujihusisha na kuiendesha taasisi ya Apps and Girls, Carolyne amejiingiza kwenye biashara ambapo ni mshirika katika uanzishwaji wa Chuo cha Nlab innovation Academy, pia ni mwekezaji katika sekta ya kilimo na mifugo. 

Anajihusisha na ukulima wa mazao ya chakula kama Alizeti na mahindi, ambapo anatengeneza Unga wa Dona na Sembe kutoka kwenye mazao ya mahindi, anatengeneza Mafuta ya Kupikia kutoka kwenye zao la Alizeti, anatengeneza vyakula vya mifugo na kujihusisha na kilimo cha Migomba.
Pia Kwa sasa Carolyne anajihusisha na uwekezaji katika sekta ya fedha, Kupitia Microfinance ya WRIS, wanasaidia biashara ndogo ndogo na watu binafsi wenye uhitaji wa fedha.


Ungependa kumfahamu nani? Tuma maoni yako kwenye barua yetu pepe nianimedia@gmail.com

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi