Kivumbi Mtaani, Wazazi wapokea Posa ya PILI, Wakwanza aenda polisi Kusimamisha Ndoa

 


Jamaa mmoja huko Vingunguti jijini Dar es salaam  alitoa posa kwa ajili ya kuoa msichana mmoja kutoka katika familia fulani. lakini baada ya kuonekana akisuasua kuoa wazazi wa msichana huyo waliamua kupokea posa ya mtu mwingine na kuruhusu binti yao aolewe.

Baadhi ya watu wa karibu na familia hiyo wamesema kuwa jamaa huyo amekuwa akiahirisha mara kwa mara suala la kuoa na baadaye akawaambia kwamba ameahirisha hana mpango wa kuoa na akagoma kurudishiwa hela aliyoitoa kwa ajili ya posa.

Siku ya ndoa jamaa huyo alikuja na Polisi na kupelekea mtafaruku mkubwa ambapo baada ya Polisi kusimuliwa kilichotokea waliwaacha waendelee na shughuli hivyo kufanya jamaa huyo akose mke, japo watu wa karibu wamesema jamaa huyo tayari ana mke wa kwanza hivyo hawajajua sababu iliyomfanya aahirishe zoezi lake la kuoa mke wa pili.


Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi