Kundi la wanamuziki kutoka Kenya ambao wamekuwa wakiiwakilisha vizuri East Africa kwenye level za Kimataifa, kwa mara nyingine tena wameandika kwenye ukurasa wa Facebook kuhusiana na video ya wimbo wao ambao ulipigwa marufuku kurushwa hewani kwenye vituo vya television Kenya.
Katika ujumbe huo ulioandikwa na wanamuziki hao wameonyesha kushukuru kwa support ya nguvu ya mashabiki wao mbali na kupigwa marufuku katika vituo vya television lakini umebakiza watazamaji wachache tu kwenye mtandao wa Youtube kufikisha idadi ya watu milioni 1 walioitazama video hiyo, hivyo huenda kuzuiwa kwa nyimbo hiyo kumeifanya ipate umaarufu zaidi na hata kuingizwa kwenye list ya zinazowania tuzo mbalimbali za Kimataifa.
Ujumbe huo kwenye Facebook unasomeka hivi; “… Morning, our forbidden fruit (Nishike) http://youtu.be/KYFQRuqQ7EM has received various international acclaim and recognition this year as well as major nominations,we won some and lost some and it’s all thanks to you#TeamSautisolfor taking your time to watch it , download and share. We’re now just a couple of views away from hitting 1M on Youtube. So, it’s our humbled request that you keep watching and sharing it with your friends#Loyalty #TeamNishike…“– Sauti Sol.