Maadhimisho ya Mwaka mmoja tangu kufariki kwa shujaa wa Afrika, Nelson Mandela…


Ni mwaka mmoja tangu Mzee Nelson Mandela alipofariki dunia, wananchi wameedhimisha mwaka mmoja toka waondokewe na kiongozi huyo ambaye aliiongoza nchi hiyo kutoka mikononi mwa Makaburu baada ya kufungwa miaka 27 jela.

Maadhimisho hayo yametanguliwa na ibada ya maombi ambapo wamekaa kimya kwa dakika tatu, na kisha kuweka mashada za maua wakiongozwa na wazee waliopigana na makaburu wakati wa utawala wa ubaguzi wa rangi, kumekuwa na upulizaji wa vuvuzela nchini kote, kugonga kengele, ngoma, na kutakuwa na mechi ya mchezo wa kirafiki wa kriketi.

Mandela alikuwa Rais wa kwanza mzalendo kuiongoza Afrika Kusini kwa kipindi cha muhula mmoja wa miaka mitano kuanzia mwaka 1994 hadi 1999 alipoachia madaraka kwa hiari yake mwenyewe.

Maduka mengi ya kuchora Tatoo Nchini humo yameripoti ongezeko la watu wanaochora Tatoo za picha ya Mandela.

“… Kimwili hatuko nae lakini kiroho Mandela tuko nae siku zote mpaka mwisho haijawahi kubadilika, Madiba kiroho tuko nae kila siku, najua Madiba anatabasam, Madiba anafurahi kwa sababu yeye ni miongoni mwa familia aliyochagua kuijenga”, alisema Mjane wa Mandela, Grace Machel.

Mshindi wa tuzo ya Amani ya Nobel, Desmond Tutu katika maadhimisho hayo ametoa wito kwa wananchi Afrika Kusini kuiga mfano wa Mandela.

Nje Ya Box

Chapisha Maoni

Mpya zaidi Nzee zaidi